• beyondgivingtz@gmail.com
  • +255761028861

Event Start Date

April 17, 2023

Event End Date

April 21, 2023

Address

Shule ya Msingi Mvuha

MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2023

Mtandao wa Elimu Tanzania (Ten/Met) kwa kushirikiana na mashirika wadau wa elimu na Serikali, wanafanya maadhimisho ya Juma la elimu limezinduliwa mkoani Morogoro, ambapo asasi za kiraia zimekumbushwa wajibu wa kuchangia juhudi za Serikali katika kuboresha elimu.

Maadhimisho haya maarufu kwa jina la Gawe, ikiwa ni kifupi cha maneno ya Kiingereza (Global Action Week of Education) yamekuwa yakifanyika kila mwaka duniani kote kuanzia mwaka 2003, yakiwa na lengo la kuwaleta pamoja wadau wa elimu katika nchi mbalimbali kujadili na kufanya jitihada za pamoja kuhakikisha wanatatua na kupunguza changamoto zinazofanya watoto wasijifunze ipasavyo wawapo shuleni.

Joseph Msuka

Maadhimisho hayo yamebebwa na kauli mbiu ‘Tuwekeze rasilimali za ndani kwenye elimu kwa maendeeo endelevu’ inayolenga kuukumbusha umma umuhimu wa juhudi za pamoja za wadau wa elimu ikiwemo Serikali, asasi za kiraia, sekta binafsi na wananchi kwa ujumla katika kuendeleza elimu.

MGENI RASMI katika maadhimisho haya ni alikua ni Mkuu wa wilaya ya Morogoro Rebecca Nsemwa ambapo amekerwa na kushuka kwa ufaulu wa wanafunzi shuleni na amewataka wazazi kuanza mara moja kuchanga chakula ili wanafunzi waanze kupata chakula shuleni.

DC Nsemwa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa Juma la Elimu Tanzania uliofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Mvuha katika Kata ya Mvuha Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro vijijini, ambapo Juma la Elimu hufanyika kila Mwaka kwa kuandaliwa na Mtandao wa Elimu Tanzania kwa kushirikiana na wadau wa Elimu na Serikali.

 

Event Location Map

Share This Event

Do you have any thing to share?