May 28, 2022
May 28, 2022
Bukandwe Secondary School (Magu)
HISTORIA YA SIKU HII
Mei 28 hufahamika kama siku ya hedhi salama duniani. Kila mwanamke hupata mzunguko wa hedhi kila mwezi kipindi, ambapo utando katika kuta za uterasi huvunjika na kutoka nje ya mwili kupitia uke wake.
WASH United ilikuja na wazo la kuadhimisha siu hii kimataifa mnamo Mei, 2013. Shirika hilo lilifanya kampeni ya siku 28 kwenye mitandao ya kijamii ili kuona kama wadau na mashirika mengine yanavutiwa na suala hili.
MWANZILISHI
Thorsten Kiefer ndiye mwanzilishi na Mkurugenzi Mtendaji wa WASH United, shirika lisilotengeneza faida nchini Berlin ambalo lilianzisha na kuratibu Siku ya Hedhi Salama ulimwenguni. Siku ya Hedhi Salama, tarehe 28 Mei huleta pamoja zaidi ya washirika 530, Taasisi za serikali, sekta binafsi, na media ili kuchochea utetezi na hatua kuelekea usimamizi mzuri wa hedhi salama kwa wanawake na wasichana wote.
Muitikio mzuri kutoka mashirika mbalimbali ulichochea kuundwa kwa maadhimisho ya siku hii kimataifa ambayo yangeruhusu wadau wote wa hedhi salama kupaza sauti zao kwa pamoja.
Wakati suala la hedhi sio jambo la aibu, bado kuna wanawake wamekuwa wakikumbana na unyanyapaa na hali ngumu ya kujimudu pindi wanapofika siku zao za hedhi.
KWANINI TAREHE 28, MEI?
Kulingana na WASH United, shirika lisilo la kujitengenezea faida na waanzilishi wa siku ya hedhi salama, kipindi cha wastani cha mzunguko wa hedhi ni siku 28. Kwa wastani, wanawake na wasichana wanapata hedhi kwa siku 5 kwa mwezi. Hivyo tarehe 28 Mei ikachaguliwa kuadhimisha siku hii.
Hivyo dhamira ya siku hii ni kuvunja ukimya kuhusu madhila yote yanayozunguka kipindi cha hedhi katika maisha ya mwanamke pamoja na kuongeza ufahamu na kubadilisha mitazamo mibaya ya kijamii kuhusu suala zima la hedhi.
USHIRIKI WA BEYOND GIVING
Hivi sasa siku ya hedhi salama haiadhimishwi na waanzilishi pekee (WASH United), lakini pia mashirika na wanaharakati mbalimbali wanaoguswa na suala hili. BEYOND GIVING Itashiriki kama Mdau na Muhamasishaji katika maswala ya hedhi na hasa kwa watoto wa kike wenye ulemavu na vile vile Tutakuwa na ugawaji wa SANITARY PADS
MGENI RASMI
Mgeni Rasmi wa sherehe hizi Atakuwa Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mh. Salim Kali
Share This Event