• beyondgivingtz@gmail.com
  • +255761028861
  • SIKU YA WALEMAVU DUNIANI

    Start Date: December 03, 2024 End Date: December 03, 2024
  • Address: Kisesa

Siku ya Kimataifa ya Watu Wenye Ulemavu, au Siku ya Walemavu Duniani, huadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Disemba. Inalenga kuongeza ufahamu wa mateso ya watu wenye ulemavu katika nyanja zote za kitamaduni, kijamii, na kisiasa huku ikikuza haki na ustawi wao katika viwango vyote vya jamii na maendeleo.

  • SIKU YA KIMATAIFA YA WANAWAKE DUNIANI

    Start Date: March 08, 2024 End Date: March 08, 2024
  • Address: Misungwi

Siku ya Kimataifa ya Wanawake, kampeni ya kila mwaka ya Umoja wa Mataifa ya kuhamasisha juhudi za kuleta usawa wa kijinsia duniani kote, mwaka huu inaadhimishwa kesho Ijumaa, kaulimbiu ikiwa ni "Wekeza kwa wanawake: Ongeza kasi ya maendeleo ."

  • MAADHIMISHO YA JUMA LA ELIMU (GAWE) 2023

    Start Date: April 17, 2023 End Date: April 21, 2023
  • Address: Shule ya Msingi Mvuha

Mtandao wa Elimu Tanzania (TEN/MET) kwa kushirikiana na mashirika wadau wa elimu na Serikali, wanafanya maadhimisho ya Juma la elimu mkoani Morogoro, ambapo asasi za kiraia zimekumbushwa wajibu wa kuchangia juhudi za Serikali katika kuboresha elimu.

  • SIKU YA MTOTO WA AFRIKA

    Start Date: June 16, 2022 End Date: June 16, 2022
  • Address: Viwanja vya Furahisha

Siku ya Mtoto wa Afrika huadhimishwa kila Mwaka tarehe 16 Juni baada ya kupitishwa kwa Azimio la nchi 51 wanachama wa Umoja wa Nchi huru za Afrika (OAU). Tanzania kama nchi mwanachama wa Umoja wa Umoja wa Afrika imekuwa ikiadhimisha siku hii tangu mwaka 1991.

  • MAADHIMISHO YA SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI

    Start Date: May 28, 2022 End Date: May 28, 2022
  • Address: Bukandwe Secondary School (Magu)

Hivi sasa SIKU YA HEDHI SALAMA DUNIANI haiadhimishwi na waanzilishi pekee (WASH United), lakini pia mashirika na wanaharakati mbalimbali wanaoguswa na suala hili. BEYOND GIVING pia itashiriki kama Mdau na Muhamasishaji katika maswala ya hedhi na hasa kwa watoto wa kike wenye ulemavu.

Do you have any thing to share?